Sarah Moses, Dodoma
MRATIBU wa Huduma za Homa ya Ini Kutoka Wizara ya Afya Barnabas Gabliel amesema hali ya ushamiri wa homa ya ini nchini ni asilimia sasa 3.5 ambayo inasababishwa na virusi vya aina B pamoja na asilimia 0.2 homa ya ini inayosababishwa na virusi aina C.
Hayo ameyasema Agosti 4 jijini Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema katika maonesho ya nane nane wanatoa huduma mbali mbali ikiwemo upimaji wa homa ya ini wa aina B lakini pia kuweza kutoa chanjo kwa wale ambao watakutwa hawana maambukizi yoyote.
Amesema kuwa kutokana na hilo wizara inawataka wananchi waweze kwenda kupima afya zao lakini pia kupata chanjo ya homa ya ini.
Lakini kwa wale ambao watakutwa na maambukizi ya homa ya ini basi tutawapeleka katika hospitali za rufaa ili waweze kupata matibabu kwani hospitali zetu za mikoa zote zinatoa matibabu.
“Ukiangalia mpaka sasa muitikio ni mkubwa kwenye utoaji wa huduma na tumefikia watu kadhaa ambayo namba itatolewa na wizara ya afya nane ili tuweze kujua mpaka sasa tumefikia watu wangapi”amesema.
Pamoja na hayo amesema kuwa maambukizi ya homa ya ini B hupatikana kwa njia ya kujamiina ,njia ya damu, njia ya kujidunga sindano kwa wanaotumia madawa ya kulevya,
Madhara ya homa ya ini kwamtu ambaye hatoweza kupata matibabu nipamoja na kupata kansa,na kifo haya ni madhara makubwa sana.
Mwisho.