Watanzania watakiwa kuonesha hamasa uzinduzi wa CHAN 2024

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WIZARA ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, imewataka wananchi kuonesha hamasa kwa kujitokeza kwa wingi katika mashindano ya CHAN 2024 yanayotarajiwa Kuzinduliwa rasmi Agosti 02, 2025 katika Uwanja wa Taifa wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Rodney Thadeus, amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mashindano hayo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza bei ya viingilio ambayo imepangwa ni rafiki na itawezesha wengi kuweza kujitokeza Uwanjani hapo kushuhudia Burudani hiyo.

Ametaja viingilio hivyo, VVIP ni Sh. 10,000 VIP B Sh. 5,000 na mzunguko ukiwa kiasi cha Sh. 2,000 huku akieleza kuwa burudani haitakuwa ya mpira pekee bali kutakuwa na wanamuziki ambao watatumbuiza Singeli.

Pamoja na mambo mengine amewasisitiza wafanyabiashara kuhakikisha wanachangamkia fursa za kibiashara ili fedha za kigeni ziweze kusali nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *