Washindi wa Shangwe la Sikikuu la LEONBET wapatikana

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya LEONBET, imewazawadia washindi wa Kampeni ya Shangwe la Sikukuu zawadi kibao kwa kushiriki kampeni hiyo.

Kampeni hiyo iliyoanza kwa kishindo hadi sasa imeshuhudia wateja wa LEONBET wakijishindia zawadi za simu janja ‘Smartphone’, Smart TV inchi 65 na Pikipiki mpya.

Mkazi wa Njombe, Freddy Mbilinyi na Juliuz Ohimo wa Kigamboni jijini Dar es Salaam kila mmoja ameshinda pikipiki mpya.

Mbali ya pikipiki, pia Mkazi wa Chamazi jijini Dar es Salaam, Ally Juma ameibuka mshindi wa Smart TV inchi 65 huku washindi wengine 15 wakishinda zawadi ya simu janja.

“Washindi hawa ni ushahidi kuwa Shangwe la Sikukuu siyo ndoto bali ni fursa halisi ya kushinda zawadi mbalimbali msimu huu wa sikukuu,” amesema Meneja Chapa wa Kampuni ya LEONBET, Lizy Ngowi.

Mmoja wa washindi, akiwa ameshikilia zawadi yake ya TV

Lizy amesema kampeni hiyo ni mwanzo tu wa msimu wa furaha kwani Shangwe la Sikukuu ndo kwanza linazidi kushika kasi na zawadi bado ni nyingi.

Amesema LEONBET imedhamiria kuhakikisha msimu huu wa sikukuu wateja wao wanaburudika ipasavyo mbali ya kushinda zawadi mbalimbali.

“Nawaomba wateja au mashabiki wa soka kubashiri na LEONBET ili kushinda zawadi nono. Kushiriki ni rahisi sana, ni kujisajili na LEONBET kupitia tovuti yetu na kuanza kubashiri kwenye mechi yoyote ama kucheza mchezo wowote unaopenda na kujiweka katika nafasi ya kushinda zawadi zetu,” amesema Lizy.

Amefafanua kuwa kila beti inakupa nafasi ya kuingia kwenye droo ya ushindi papo hapo.

“Usikubali msimu huu wa sikukuu upite bila kujishindia zawadi nono. Jiunge na familia ya LEONBET leo na ufurahie msimu wa sikukuu kwa namna ya kipekee,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *