Washindi wa Betika Mtoko wa Kibingwa wakoshwa na dabi ya K’koo

Na Mwandishi Wetu

ACHANA na ushindi wa bao 1-0 wa timu ya Yanga SC dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki, washindi wa Betika Mtoko wa Kibingwa ambao ni wanazi wa timu hizo wameizungumzia dabi hiyo huku wale wa Yanga wakitambia ubora wa kikosi chao.

Yanga iliondoka na alama tatu katika mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Bao la kujifunga la dakika ya 86 kutoka kwa beki, Kelvin Kijiri wa Simba, akiwa katika harakati za kuondosha hatari golini kwake, lilitosha kuipa Yanga ushindi huo.

Miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliokuwa uwanjani kuishuhudia dabi hiyo ni washindi wa Promosheni ya Betika Mtoko wa Kibingwa kutoka mikoa mbalimbali nchini, ambao wametoa tathimini yao huku wale wa Simba wakieleza kilichowanyima pointi.

Wakizungumza na Mtandao wa Tanzania Leo wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNIA) jijini Dar es Salaam, kabla ya kuondoka kurejea makwao, mabingwa hao kwa nyakati tofauti wamesema ilikuwa ni mechi nzuri na bora kwa kila upande.

“Ingawaje Simba tumefungwa, lakini si kwa uwezo wa wapinzani wetu, tumejifunga ni bahati mbaya katika mchezo, lakini kilichofanyika uwanjani kila mmoja amekiona,” amesema Ramadhani Liganga wa Mtwara ambaye ni shabiki wa Simba.

Shabiki wa Yanga, Shomari Makota kutoka Lindi amesema, uwezo wa wachezaji wao ndiyo chachu ya matokeo hayo hata kama Simba imejifunga kauli sawa na iliyotolewa na Rose Mgala wa Dodoma ambaye pia ni shabiki wa Yanga.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Betika, Rugambwa Juvenalius, amesema baada ya dabi hiyo iliyowapa fursa washindi wa promosheni ya Kibingwa kuishuhudia laivu kwa hadhi ya VIP, wanakuja na promosheni nyingine kubwa kwa wananchi.

“Kama kawaida yetu ni bandika, bandua baada ya Mtoko wa Kibingwa uliowaleta kwa ndege mabingwa wetu kutoka mikoa ya Mwanza, Dodoma, Mtwara, Tabora, Kagera, Katavi, Mbeya, Morogoro, Arusha na Mafia na kuungana na wale wa Dar es Salaam kuishuhudia dabi hii kwa hadhi ya VIP, sasa wajiandae kwa mambo makubwa zaidi,” amesema.

Baadhi ya mabingwa wa Betika Mtoko wa Kibingwa kutoka kwenye mikoa ya Mwanza, Dodoma, Mtwara, Tabora, Kagera, Katavi, Mbeya, Morogoro, Arusha na Mafia, waliokuja kuishuhudia dabi ya watani wa jadi, timu za Simba na Yanga mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam

Pia Balozi wa Mtoko wa Kibingwa, Baraka Mpenja amesema, msimu huu wa nane imetoa washindi 500 wa zawadi mbalimbali ikiwamo kuishuhudia dabi.

“Ilikuwa ni rahisi kushinda kwa kuweka mkeka wenye mechi 3 au zaidi kwa sh. 1000 na kubeti kwa kupiga *149*16# au www.betika.co.tz.

“Kulikuwa na zawadi mbalimbali za siku, wiki na mwezi ikiwamo fedha taslimu na fursa ya kuishuhudia laivu dabi kwa hadhi ya VIP gharama zote zikitolewa na Betika,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *