Wananchi watakiwa kujitokeza kupata msaada wa kisheria

Sarah Moses, Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesema kuwa kupitia msaada wa kisheria wa Mama Samia (Mama Samia Legael Aids Campain ) Wizara ya Katiba na Sheria inatakiwa kujitangaza zaidi ili wananchi waweze kujitokeza kupata elimu lakini pia msaada wa sheria.

Hayo ameyasema leo Agosti 5,2025, Jijini Dodoma wakati alipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria kwenye maonesho ya siku ya wakulima (nane nane) .

Amesema kuwa wanahitaji wananchi wanufaike na sheria kwani wengi wao wanaowafata wanakuwa hawajui sheria nakuomba washauriwe mambo ya kisheria.

Kwaupande wake Mkurugenzi Msaidizi Ufuatiliaji na Uzingatiaji  wa Msaada wa Kisheria Osborn Paiss amesema kuwa wanaendelea kutekeleza kampeni ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia lakini pia  kutoa elimu kuhusiana na  utajiri na maliasili za nchi ambazo nimojawapo ya kazi zinazofanywa na Wizara ya Katiba na sheria.

“Lakini pia tunatembelewa na wananchi ambapo tunawapa ushauri mbalimbali ikiwemo mirathi, ardhi na mashauri ya ndoa”amesema Paiss .

Pamoja na hayo amesema kuwa Wanaendelea kujitangaza na kuwasihi wananchi waweze kufika katika eneo hilo ili waweze kupata msaada wa kisheria.

“Tunawakaribisha kwa wingi ili tuweze kuwasaidia kuwapa elimu kuhusu masuala mbalimbali ambayo yanawazunguka katika maeneo yao”

Hata hivo amesema kuwa huduma hizo wanazitoa bure na Mawakili wapo lakini pia wataaalam wengine wa maeneo mbalimbali ambayo wanafahamu kwamba yanakuwa yanawagusa moja kwa moja.

Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *