Waganda wawili waondoka na Yanga kujaribiwa Malawi

Na Zahoro Mlanzi

WAKATI timu ya Yanga, ikiwa imeondoka nchini muda si mrefu kwenda Malawi kunogesha Sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa nchini hiyo, nyota wawili raia wa Uganda, Sharrif Kimbowa na Moses Aliro, wapo katika msafara huo kwa ajili ya kufanyiwa majaribio.

Nyota hao wamekuja kufanya majaribio na wakionesha kiwango kizuri watasajiliwa.

Timu hiyo imeondoka na ndege maalum ambapo kesho itacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Nyasa Big Bullets ya nchini humo baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa marais ambao wamealikwa katika sherehe hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *