‘VAR’ kuanza kutumika Ligi Kuu Bara

Na badrudin Yahaya

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeipa nchi ya Tanzania video za usaidizi wa marefa (VAR) ambazo zitafungwa nchini kwenye viwanja vyenye ubora.

Hayo yamethibitishwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia wakati akitoa hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo uliofanyika mkoani Iringa.

Karia amesema tayari wataalamu wa kufunga vifaa hivyo na kutoa mafunzo wameshafika nchini tangu jana na kazi itaanza hivi karibuni.

Aidha amesema kupewa vifaa hivyo ni kutokana na ushirikiano mzuri kati yao na CAF.”

Hivi karibuni tutaanza zoezi la kufunga VAR, wataalamu wameshafika tangu jana,” amesema.Zoezi hilo linatarajia kufanyika katika viwanja ambavyo vimekizi vigezo vya CAF ikiwemo Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Tanzania ikifanikiwa kufunga VAR itaungana na nchi zingine za Afrika kama Misri, Algeria na Morocco ambazo tayari zinatumia kifaa hicho.

Katika hatua nyingine, CAF, imemteua Rais wa Yanga na Mwenyekiti wa Shirikisho la Klabu Afrika, Injinia Hersi Said, kuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya michuano ya Afcon na Chan.

Akizungumza uteuzi huo katika Mkutano huo,Karia amesema Hersi ameingia katika kamati hiyo kwasababu ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji CAF ambao ameupata baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa ACA.

“Kwa nafasi ya kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa CAF baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ACA, moja kwa moja ndugu Hesri anakuwa mjumbe wa kamati ya maandalizi ya michuano ya Afcon na Chan,” amesema.

Hersi ameshinda nafasi hiyo mapema mwezi huu katika uchaguzi ambao ulifanyika nchini Morocco huku yeye akiweka historia ya kuwa mwenyekiti wa kwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *