Ugonjwa wa mlipuko wawaua 11 Uganda



Na BBC

MAOFISA wa Afya nchini Uganda, wanachunguza mlipuko wa ugonjwa usiojulikana ambao umewaua takribani watu 12 katika kipindi cha wiki mbili zilizopita katika Wilaya ya Kyotera iliyoko katikati mwa Uganda

Waathiriwa wa ugonjwa huo wanatokea vipele mwilini ambavyo vinasambaa na kuwa vidonda kabla ya kufariki dunia baada ya kuugua kwa siku chache huku wengine wakionesha dalili za kuvimba viungo vya mwili.

Wizara ya afya Uganda imechukua sampuli ya ngozi ya mmoja wa wagonjwa aliyefariki ili kufanyia vipimo.

Matokeo yake bado hayajatangazwa kwa umma.

Maofisa wa afya wa eneo hilo wanaonya kuwa imekuwa vigumu kudhibiti hali kwani baadhi ya wagonjwa wanakimbilia kwa waganga wa kienyeji badala ya kwenda hospitali.

Mwisho

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *