Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kuchunguza tuhuma za Gekul

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekusudia kufanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma za ukatili na udhalilishaji unaodaiwa kufanywa na Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul dhidi ya Hashim Ally mkazi wa Babati Mjini, mkoani Manyara.

Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Mohaned Hamad aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema taarifa za kitendo hicho zimekuwa zikisambaa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii hivyo tume imeamua kufuatilia kwa kina ili kupata usahihi wa taarifa hizo.

Alieleza kuwa, pamoja na hatua zilizochukuliwa na Mamlaka mbalimbali, THBUB imeona kuna haja ya kufanya uchunguzi huo kwa mujibu wa ibara ya 130 (1) (c) na (f) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977, kifuungu cha 6 (1) c, f, g na kifungu cha 15 (1) (a) vya Sheria ya THBUB, sura ya 391 ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo.

Aliongeza kuwa, Ally alikamatwa, kujeruhiwa sehemu mbali mbali za mwili wake akiwa katika mazingira ya kazini kwake jambo ambalo limesababisha apate maumivu makali katika mwili wake.

“Kama inavyoelezwa na vyombo vya habari, Ally alikamatwa, kupigwa, kujeruhiwa na kuwekewa chupa katika eneo la haja kubwa akiwa kazini kama mtumishi wa Paleii Lake View Garden, inayodaiwa kumilikiwa na Mbunge huyo” alisema Makamu Mwenyekiti.

Hata hivyo, alisema chanzo cha udhalilishaji huo kinadaiwa ni kutumwa na mshindani wa kibiahara wa Mbunge huyo kumuwekea sumu na kumuua.

Tuhuma hizo ziliibuka Novemba 25, 2023 baada ya kusambaa kwa video mitandaoni ikimuonesha Ally akielezea ukatili na udhlilishaji aliofanyiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *