TTCL mbioni kufikisha huduma zake Kongo

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania(TTCL), linaendelea na mchakato wa kufikisha huduma zake nchi jirani ikiwamo Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo.

Mtendaji wa Kampuni Tanzu ya TTCL(T-PESA), Lulu Mkudde, ameeleza mpango mkakati huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye banda lao katika Maonesho ya 48 Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayofikia tamati leo Julai 13,2024.
Amesema mpaka sasa huduma hiyo imefikishwa katika nchi nne ikiwemo Burundi, Rwanda, Zambia na Malawi.

“Tunaposema tunafungua milango ya kidigitali inamaanisha kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi katika kutumia huduma za intaneti katika kutekeleza huduma mbalimbali kwa watu wengine,”amesema Lulu.

Ameongeza kuwa hadi sasa shirika limefanya mambo mbalimbali ikiwamo huduma ya TTCL – Pesa.

Amesema katika maonesho hayo wametoa huduma ya Akaunti Pepe inamuwezesha mteja kufungua akaunti yake bila hitaji, mteja anauwezo wa kutumia akaunti yake saa 24 kwa siku,”amesema.

Ameongeza kuwa hadi sasa, shirika limesambaza Mkongo wa Taifa katika mikoa yote nchini ambapo zaidi ya wilaya 98 zikiwa zimefikishiwa mkongo wa mawasiliano.

Lulu alisema juhudi hizo zote zinalenga kuhakikisha huduma za elimu, afya na maendeleo ya kiuchumi ambayo yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini.

Akizungumzia Huduma ya T-cafe, Mkudde amesema ina ya WiFi ambayo ina waondolea adha wafanyabiashara, waandishi wa habari na wataalamu wa masuala ya ushauri katika kufanya kazi zao wakiwa nje ya ofisi.

Amesema ni huduma ambayo inasaidia mtu yoyote kufanya kazi nje ya ofisi kwa kupata uwezo wa kutumia huduma zao katika kutekeleza huduma zake .

“Shirika limeanzisha huduma hii ili kuwawezesha wateja wote kufanya shughuli zao kwa haraka na gharama nafuu,ambapo kwa kipindi hiki cha Sabasaba tumeshuhudia huduma hii inavyofanya kazi kwa speedi ya hali ya juu na wananchi kwa wakati wote walikuwa wakitumia katika maonesho hayo,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *