Trilioni 11.4 kutekeleza miradi ya maendeleo Kigoma

Na Sarah Moses, Dodoma.

MKOA wa Kigoma umepokea kiasi cha shilingi trilioni 11.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya  maendeleo ambayo baadhi imekamilika na mingine ikiendelea na utekelezaji huku mingine ikiwa katika mchakato kuelekea kuanza kutekelezwa. 

Hayo ameyasema leo julai 19 Balozi Saimon Sirro wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita ambapo amebainisha kuwa pato la mwananchi limeongezeka kutoka shilingi 1,448,134 mwaka 2020 hadi shilingi 2,105,770 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 45.4.

Miradi hiyo ni pamoja na Reli ya SGR (Tabora hadi Kigoma na Uvinza hadi Msongati – Burundi, Ujenzi wa nyumba za Viongozi na Ofisi ,Elimu ,Ukarabati na uboreshaji wa uwanja wa ndege Kigoma ,Afya .

“Ujenzi wa barabara, Miradi ya meli Msongati –Burundi) Nishati na Miradi ya maji” amesema

Amesema kuwa mafanikio waliyoyapata Kigoma kupitia TANROADS  kwa mwaka 2020 hadi 2025 ni pamoja na kufanikiwa kukamilisha barabara ya Kasulu–Kabingo (km 184), ujenzi wa daraja la Malagarasi katika barabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu.

” kilomita 8.35 za lami kati ya kilomita 25.9 barabara ya Nduta Junction – Kibondo Mjini na ujenzi wa barabara ya Kibondo – Mabamba uliofikia asilimia 32″ amesema.

Katika kipindi cha mwaka 2020 hadi  2025, TARURA  imefanikiwa kuongeza barabara za kiwango cha lami kutoka kilomita 53.744 na kufikia kilomita 100.675.

Lakini pia  wameongeza barabara za kiwango cha changarawe kutoka kilomita 619.291 hadi kufikia kilomita 1,302.55 na kuongeza madaraja na makalavati kutoka 92 na 1,142  hadi kufikia 130 na 2,071 mwaka 2025 kwa mfuatano huo.

Vilevile amesema jumla ya barabara zenye hali nzuri zimeongezeka kutoka kilomita 1,222.436 mwaka 2020 hadi kufikia kilomita 1,860.554 mwaka 2025, barabara zenye kiwango cha zege kutoka kilomita 1.02 hadi kufikia kilomita 6.89 mwaka 2025 na madaraja ya mawe kutoka 49 mwaka 2020 hadi kufikia 150 mwaka 2025.

Katika hatua nyingine Balozi huyo amesema kuwa mkoa umepokea shilingi bilioni 50.928 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za afya .

Fedha hizo zimeimarisha miundombinu ya kutolea huduma za afya, imeongeza upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba, vitendanishi na imeimarisha upatikanaji wa karibu wa huduma za afya.

“Upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya umeongezeka kutoka asilimia 86 mwaka 2020 hadi asilimia 92 mwaka 2025” amesema.

Hata hivyo amesema kuwa Hospitali za wilaya zimeongezeka kutoka tatu mwaka 2020 hadi nane mwaka 2025, vituo vya afya kutoka 34 hadi 53, idadi ya zahanati kutoka 236 hadi 283 na nyumba za watumishi wa afya kutoka 384 hadi 416.

Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *