Toure ataka Kane abaki Spurs

LONDON, England

NYOTA wa zamani wa Manchester City, Yaya Toure, amemshauri Harry Kane kubakia ndani ya Tottenham kwa maisha yake yote ya soka yaliyobakia.

Hatma ya nahodha huyo wa England, imekuwa katika wakati mgumu kipindi hiki na Kane amekuwa akihusishwa kujiunga na Manchester United au Bayern Munich.

Spurs imekuwa ikisisitiza haitomuuza nyota wake huyo licha ya kwamba anaingia mwaka wa mwisho katika mkataba wake, huku Toure akifikiri Kane anapaswa kumalizia soka lake ndani ya klabu hiyo ya utotoni.

Toure alipata nafasi kushuhudia karibu robo nzima ya maisha ya Kane wakati akifundisha timu yao ya vijana na kutambua kipaji chake.

“Harry Kane ni mchezaji mzuri na kiongozi wa kipekee,” alisema kiungo huyo, 40, ambaye ameamua kufundisha soka ndani ya timu ya Standard Liege, alipozungumza na Shirika la Habari la PA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *