Tigo yawekeza trilioni 1 kuboresha mtandao wake

Sarah Moses,Dodoma.

MKURUGENZI wa Tigo Kanda ya Kati Said Iddy amesema kuwa Tigo Tanzania imewekeza zaidi ya Trilioni moja katika kuboresha mtandao wake,ambapo kwa sasa inaongoza kwa ubora nchini nahivyo kusaidia wafanyabiashara na wakulima kupata taarifa kwa urahisi zaidi za kilimo .

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Agosti 5,2024 katika viwanja  vya maonyesho ya Kimataifa ya wakulima nanenane yaliyopo Nzuguni Jijini Dodoma amesema maboresho hayo  yatarahisisha upatikanaji wa masoko ya wakulima na hivyo kuchangia kwa kasi kubwa  maendeleo ya watanzania.

Amesema lengo la kuboresha mtao wao ni kurahisisha mawasiliano ya wananchi lakini pia kuweza kuwapa fursa wananchi kutumia mtandao huo katika shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo “ukilima bidhaa unataka kwenda kuuza bidhaa ambapo inapelekea kupata masoko ambayo yanakulazimu kutumia matandao wa tigo ambao upo kasi zaidi”.

“Lakini pia tunayosimu ya bei rahisi Tanzania ambayo haijawahi kutokea kwani mteja analipa kiasi cha shilingi 35,000 tu halafu inayobaki analipa kidogo kidogo shilingi 650 kwa siku hivyo mwananchi wa kawaida anaweza kumudu kulipia simu hii na akaitumia na mtandao watigo katika shughuli za kimaendeleo” amesema Mkurugenzi huyo.

Akizungumzia taarifa na usalama wa fedha za mteja Iddy amesema kuwa kwao ni kipaumbele kwani wamekuwa wakijikita katika kutoa elimu kwa wananchi na wateja wao kwa kuhakikisha kwamba namba  rasmi inayopiga kwa mteja ni namba 100,kwahiyo namba yoyote itakayopiga tofauti na hiyo wasitoe ushirikianao kwasababu inakuwa haijatoka tigo.

Hata hivyo amesema kuwa katika msimu huu wa nanenane Tigo Tanzania inaendelea na kampeni yake ya Sako kwa Bako ambayo inatoa dakika na MB za ziada kwa mteja wa tigo,nakuongeza kuwa kampeni hiyo haibagui mteja wa tigo kwani ananafasi ya kujishindia dakika mpaka 100 na MB kadhaa kwakila anaponunua kifurushi chake lakini pia anapata MB ambazo anatumia kwenye mtandao wa WhatsApp bure kwa masaa 24 na kuendelea.

Mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *