Na Asha Kigundula
WAKATI timu ya Azam FC, ikiondoka nchini leo mchana kwenda kuweka kambi nchini Tunisia, Kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’, amesema mechi yao dhidi ya Yanga ya Ngao ya Jamii itakuwa ngumu.
Kauli hiyo aliitoa baada ya kuulizwa wanaenda kuweka kambi nchini Tunisia na wakirudi mechi ya kwanza, watakutana na Yanga katika nusu fainali ya Ngao ya Jamii.
Fei Toto akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akizungumza na gazeti hili, amesema:”Sio Yanga tu, timu yoyote tutakayokutana nayo tutapambana nayo.
Ameongeza anaamini itakuwa mechi nguvu kuikabili Yanga lakini wana imani maandalizi watakayofanya yatawasaidia kupata matokeo mazuri.
Akizungumzia kuhusu kocha wake mpya, Msenegal, Youssouph Dabo kwa siku chache alizofanya nawe mazoezi Chamazi Complex, amesema ana mazoezi mazuri na watafika mbali.