TCAA: Ndege iliyoanguka Mkuranga lilikuwa jaribio la uokoaji

Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam 

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga (TCAA) imewatoa hofu wananchi kuhusu taarifa za ajali ya ndege iliyotokea Jumatano Julai 26, 2023 katika kijiji cha Msufini kilichopo Mkuranga mkoani Pwani kuwa ilikuwa ni zoezi la kupima uwezo wa utayari katika kukabiliana na matukio ya utafutaji na uokoaji wa ndege zinazopata ajali.

Ndege aina ya Embraer 120 (E120) iliyokuwa imebeba abiria 25, ilihusika kwenye mazoezi hayo na ilikuwa imetoka uwanja wa Kilwa Masoko ikielekea uwanja wa Tanga.

“Waangalizi hao ni kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO), Mashirika ya ndege ya ndani na nje ya nchi, Chuo cha Bandari Dar es Salaam (DMI) na mashirika ya vyombo vya majini. Waangalizi hawa watatoa ripoti ambazo zitafanyiwa kazi na kamati ya kitaifa ya utafutaji na uokoaji wa ajali za ndege na vyombo vya majini.

“Napenda kutoa taarifa kwamba kilichofanyika kilikuwa ni zoezi ambalo lengo lake ni kupima uwezo na utayari wetu kama nchi wa kukabiliana na matukio ya utafutaji na uokoaji wa ndege zinazopata ajali kwenye nchi kavu na majini na pia vyombo vya majini,” amesema.

Amesema zoezi hilo limehusisha waangalizi wa ndani na nje ya nchi ili kutathmini maeneo yanayohitaji kuboreshwa ili huduma itolewe kwa ufanisi. Waangalizi hao ni kutoka Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga duniani (ICAO).

Naye Mkurugenzi Huduma za Uongozaji wa Ndege wa TCAA, Flora Mwashinga amesema baada ya mazoezi hayo, Shirika la Kimataifa la Usafiri  wa Anga Dunia (ICAO) limeishauri TCCA na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kuboresha mifumo yao ili kuweza kurahisisha zoezi la utafutaji na uokoaji wakati ajali za ndege na vyombo vya majini zinapotokea. 

Amesema katika zoezi hilo ambalo lilikuwa likifuatiliwa na Shirika hilo la Usafuri wa Anga Duniani wamebaini uwepo wa changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha zoezi la uokoaji hivyo kushauri namna ya kuweza kufanyiwa kazi.

“Katika kuhakikisha tunatatua changamoto hiyo tupo katika mchakato wa kuwa na sheria mama ya utafutaji na uokoaji, ili iweze kusaidia TASAC na TCAA kufanya kazi kwa ufanisi wakati wa kufanya ufatiliaji na uokoaji pindi ajali za ndege zinapotokea,” amesema.

Ameongeza kuwa TASAC na TCAA ni taasisi ambazo zinafanyakazi kwa miongoni tofauti ya kimataifa lakini inawahitaji linapotokea tatizo la ajali waweze kuratibu tukio zima kwa pamona hivyo kitu ambacho kitawaongoza kufanya hivyo ni uwepo wa sheria moja ambao itasimamia suala la utafutaji na uokoaji.

“Tulishaanza mchakato wa kutengeneza hiyo sheria sasa hivi tupo kwenye hatua ya kati ya kuitengeneza, uwepo wa sheria hii  itawezesha kufanya kwa urahisi suala zima la utafutaji na uokoaji wakati ajali za ndege  itakapotokea ,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *