Na Eckland Mwaffisi, Dar es Salaam
KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyrara, amesema Serikali ya Tanzania ikishirikiana na Serikali ya China inatarajia kuliboresha Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TARAZA).
Lengo ni kuliwezesha shirika hilo kuongeza ufanisi hasa jatika usafirishaji wa mizigo.
Prof. Kahyrara aliyasema hayo jijini Dodoma jana wakati akisaini mkataba wa utendaji kazi na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Alisema tija ya maboresho hayo ni pamoja na kukuza pato pato la taifa, urahisi kwenye usafirishaji mzigo kutoka eneo moja kwenda jingine.
“Shirika la TAZARA ni moja ya mashirika ambayo yanapewa kipaumbele kwa sasa hasa katika uboreshaji wa miundombinu ambayo kwa muda mrefu haikukarabatiwa.
“Wenzetu wa Serikali ya China wameonyesha nia ya kusaidia kwenye eneo hilo,” aliusema Prof. Kahyrara.
Aliongeza kuwa, tayari Serikali imefanya maboresho katika Sheria ya Reli ili kuruhusu sekta binafsi kutoa huduma katika Reli ya TAZARA na TRC.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TRC, Masanja Kadogosa, alisema miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa katika reli ya kati na ya kisasa ambayo hivi karibuni majaribio yatafanywa, kuanza kutoa huduma.
Kadogosa aliongeza kuwa, vitendea kazi kwa ajili ya uendeshaji SGR vimeendelea kuwasilia, tayari TRC imepokea kichwa kimoja cha reli hiyo kutoka Korea Kusini ambapo ni miongoni mwa vichwa 17 ambavyo vimeagizwa.
Mkurugenzi wa Tathimini na Ufutiliaji kutoka Wizara ya Uchukuzi, Devota Gabriel, alimuhakikishia Prof. Kahyarara kuwa, kitengo hicho kimewekea mikakati thabiti itakayowezesha wataalam wa Wizara kusimamia kwa karibu miradi iliyopangwa kutekelezwa mwakawa fedha 2023/2024 ili kuzingatia thamani na ubora.