Sh. bilioni 9 kutekeleza miradi 7 ya maji Mtwara

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

SERIKALI imetoa Shs. bilioni 9.8 ili kutekeleza miradi saba ya maji katika Wilaya za Mtwara na Tandahimba mkoani Mtwara.

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mtwara, Primi Damas, aliyasema hayo jana katika hafla ya kusaini mikataba ya utekelezaji wa miradi hiyo kati ya wakala huo na Wakandarasi.

Alisema utekelezaji wa miradi hiyo utawanufaisha wakazi  67,149 wa vijiji 35.

Aliongeza kuwa, kukamilika kwa miradi hiyo kutaongeza upatikanaji maji kwa asilimia 17 Wilaya ya Tandahimba na asilimia 5.8 kwa Wilaya ya Mtwara.

Mkuu wa Mkoa huo, Kanali Ahmed Abbas aliishukuru serikali na kuwataka viongozi wa Wilaya hizo kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na ubora unaoendana na thamani ya pesa iliyotolewa.

“Miradi hii ni mikubwa, viongozi simamieni ili ukamilikaje wake utatue changamoto ya maji kwa Mkoa wetu,” alisema Kanali Abbas.

Aliwataka Wakandarasi waliosaini mikataba hiyo kwenda eneo la kazi, kuanza kazi, kuhakikisha miradi inakamilika ndani au kabla ya muda uliowekwa kwenye mikataba. Mikata yote iliyosainiwa inatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *