Serikali yawaandalia zawadi maalum Simba Queens

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema imefurahishwa na matokeo ya timu ya Simba Queens na kwamba imepanga kuwafanyia kitu mara baada ya kuwasili wakitoka kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki.

Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi fedha timu ya Yanga SC, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, alisema Serikali ipo kwa ajili ya michezo yote.

Msigwa alisema wamefurahishwa na matokeo ya Simba Queens, lakini haikuwa sehemu ya mpango wa ‘Goli la Mama’, lakini kwa kutambua thamani yao wameamua kuwaandalia zawadi maalum.

Alisisitiza ‘Goli la Mama’ limewekwa kwa ajili ya timu zinazoshiriki Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

(Kwa taarifa zaidi usikose kusoma nakala yako ya Gazeti la Tanzania Leo kila Jumatatu hadi Ijumaa)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *