
Na Mwandishi Wetu, Mara
SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. samia Suluhu Hassan imetoa kiasi Sh. bilioni 5.7 kwa ajili ya ujenzi wa shule mbili mkoani Mara ambazo ni shule ya Sekondari ya Wasichana Mara pamoja na shule ya Amali Butiama (Butiama Technical Sec School).
Fedha hizo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa shule hizo mbili ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Ubora wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP) mkoani Mara kwaajili ya kutekeleza ilani ya uchaguzi ya ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka (2020-25) kuhusu kuongeza uandikishaji wa wananfunzi wa wanafunzi kidato cha kwanza hadi kidato cha nne pia kidato cha tano na sita.
Kati ya fedha hizo jumla ya Sh. bilioni 4.1 zimetolewa kwaajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika Shule ya Sekondari ya Mara wasichana iliyojengwa katika Kijiji cha Bulamba kKata ya Butimba wilayani Bunda.
Katika shule ya Sekondari ya Mara wasichana serikali imekamilisha miundombinu mbalimbali ikiwamo jengo lenye vyumba vya madarasa mawili, Majengo matatu yenye vyumba vya madarasa mawili na ofisi moja, madarasa mawili na vyoo, maabara ya fizikia na chumba cha Jiografia, Maabara ya Kemia na Biolojia, Jengo la utawala, vyoo vya wanafunzi matundu 16, chumba cha jenereta, Bwalo, Nyumba ya mwalimu yenye vyumba 3, vyumba ya mwalimu (2 in 1), mabweni manane, jengo la wagonjwa pamoja na ujenzi wa uzio.
Katika hatua nyingine serikali imetoa kiasi cha Sh. bilioni 1.6 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Amali Butiama (Butiama Techinacal Sec School) wenye jumla ya majengo 18.
Fedha hizo zinaendelea kutumika kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vinne (04) vya madarasa bila ofisi, vyumba vinne vya madarasa na ofisi, Jengo la utawala na stoo ya site, maabara mbili, kemia na baiolojia, nyumba moja ya mwalimu(single), makataba moja, chumba cha TEHAMA kimoja, mabweni manne, bwalo na jiko, vyoo matundu manane, karakana ya mechanics & Metal fabrications, karakana ya ufundi uashi na tanki la maji.

