Scott: Fury avuliwe ubingwa wa Dunia

LAS VEGAS, Marekani

BONDIA wa uzito wa juu, Tyson Fury, amekumbana na wito wa Kocha wa Deontay Wilder wa kunyang’anywa taji lake la Dunia huku kukiwa na tetesi za pambano la Francis Ngannou.

Fury na Ngannou, wanatarajia kutangaza uwepo wa pambano lao wiki hii, linaloaminika halitakuwa la ubingwa.

Hilo limemfanya Kocha wa Wilder, Malik Scott, kuchukizwa na kushinikiza kwa WBC kuchukua hatua kwa kumvua ubingwa bingwa huyo wa Dunia.

Scott alizungumza na ESNEWS: “Acha Deontay na [Andy] Ruiz wapambane kwa ajili ya WBC.

“Hebu tufanye kitu kinachoeleweka, kitakachosaidia michezo. Achana na pambano la kipumbavu linalosubiriwa kati ya Fury na Ngannou kupambana.

Fury, 34, ameshindwa kufikia mwafaka wa kuzichapa na Oleksandr Usyk, 36, mwaka huu katika kile kilichotajwa ni pambano la kwanza kuhusishwa mikanda minne katika uzito wa juu.

Kwa sasa Usyk anatetea mikanda yake Agosti 26 kwa kuzichapa na mpinzani wa lazima, Daniel Dubois, 25, nchini Poland.

Wakati huohuo, Anthony Joshua, 33, atarejea ulingoni katika pambano la marudiano Agosti 12 dhidi ya Dillian Whyte, 35.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *