Satar-Haji ampa ushauri Rais mpya ZFF

Ibrahim Nyakunga

ALIYEKUWA Mgombea wa Uraisi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF), Kamal Abdul Satar-Haji, ameshauri Rais wa ZFF, Suleiman Mahmoud Jabir kutengeneza ofisi ya shirikisho hilo.

Kamal ambaye katika uchaguzi huo, alishika nafasi ya pili akiwa na kura 15, huku akizidiwa kura moja na Rais wa sasa, Suleiman Mahmoud Jabir aliyepata kura 16 wakati mgombea wa tatu, Juma Hassan Thabiti hajapata kitu.

Akizungumza na gazeti hili leo, Satar-Haji, amesema itakuwa jambo zuri kabla Rais Jabir hajaanza kufanya mambo mengine
angehakikisha anatafuta wadhamini ili ajenge ofisi.

Amesema ofisi ndiyo itamsababishiaa kufanya mambo yake kwa wepesi na kutekeleza ahadi zake kwa urahisi kwani atakuwa na sehemu ya nzuri ya kufanyia kazi .

Amesema yupo tayari kushirikiana na rais huyo kwa kila jambo ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika soka la Zanzibar.

“Mimi kabla sijagombea urais nilikuwa natoa msaada na hata sasa hivi nitaendelea kutoa misaada kwa sababu lengo ni kuleta maendeleo katika soka la Unguja na Pemba na si uongozi,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *