Rooney: Maguire ondoka United

MANCHESTER, England

KUONDOKA ndani ya kikosi cha Manchester United ndio “kitu bora” kwa Harry Maguire baada ya kuvuliwa unahodha ndani ya timu hiyo, amesema straika huyo wa zamani wa United, Wayne Rooney.

Maguire, 30, amevuliwa unahodha wa ndani ya United baada ya msimu uliopita kuanza mechi nane za Ligi Kuu England.

Beki huyo amesajiliwa kwa pauni milioni 80 kwa mkataba ambao unaisha 2025, lakini nyota huyo wa Uingereza amekuwa akihusishwa kutakiwa na West.

“Kitu kizuri kwake kwa sasa ni kuondoka ndani ya kikosi hicho,” amesema Rooney akizungumza na Athletic.

“Kuvuliwa unahodha, unawezaje kusonga mbele ndani ya klabu hiyo?

“Hiyo ni wazi inaonesha kocha hakuamini. Imemfanya Harry kuwa katika nafasi ambayo afikirie jinsi ya kusonga mbele. Kocha ameonesha si sehemu ya mipango yake.

“Nina uhakika Harry anataka kuondoka aende kucheza, kwa ajili ya hatma yake ya soka England ili ajiweke katika nafasi nzuri ya kupata mafanikio kadri atakavyoweza.”

Kocha wa United, Erik ten Hag, amesema bado hajateua nahodha mpya lakini Rooney ambaye ndiye mfungaji bora wa muda wote ndani ya klabu hiyo, anaona kuna nafasi ya kupewa mwingine.

Rooney ambaye kwa sasa ndiye Kocha wa DC United, amesema ni wakati sahihi kwa kipa wa kimataifa wa Hispania, David de Gea kuondoka ndani ya klabu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *