MANCHESTER, England
MCHEZAJI wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, ana matumaini kipaji cha Marcus Rashford, kinaweza kurudisha mataji ndani ya timu hiyo na kumfanya kuwa katika kiwango sawa na nyota kama Kylian Mbappe na Erling Haaland.
Timu hiyo iliyotwaa mataji 20, imeshindwa kutwaa taji la Ligi Kuu England kwa muongo sasa, huku majirani zao Manchester City wakitawala soka la ndani kwa kipindi hicho.
United imekuwa na wakati mgumu tangu Rooney alipoondoka kwa kumsaidia Sir Alex Ferguson kutwaa taji msimu wa 2012-13 lakini mambo yanaonekana kutia matumaini chini ya Kocha, Erik ten Hag.
Mchezaji Mason Mount, alijiunga nao akitokea Chelsea na kipa wa Inter Milan, Andre Onana akijiandaa kutua Old Trafford wakati kocha huyo wa kimataifa wa Uholanzi akiendelea kukiimarisha kikosi chake ambacho kilitwaa Carabao Cup na kushika nafasi ya tatu EPL.
United imeendelea kuongezwa nguvu baada ya juzi nyota wao Rashford, kuongeza mkataba wa miaka mitano baada ya kufikisha mabao 30 kwa mara ya kwanza msimu uliopita.
“Nafikiri Ten Hag ameanza vizuri tangu alivyotua msimu uliopita,” amesema Rooney, ambaye ndiye kinara wa upachikaji mabao wa muda wote ndani ya klabu hiyo.
“Unaweza kuona jinsi anavyojaribu kutengeneza kikosi na moyo wa ushindi kutokana na usajili anaofanya, alionesha msimu uliopita na nina imani atajaribu tena mwaka huu.
Ciao…