Rais Samia atoa tiketi elfu 5 kwa mashabiki kushuhudia Yanga fainali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amelipia jumla ya tiketi 5000 kwa mashabiki wa soka nchini watakaokwenda kushuhudia mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya USM Alger utakaopigwa Mei 28, 2023 kwenye dimba la Mkapa, Dar es Salaam.

Huu ni mwendelezo wa hamasa ya Rais Samia kwa Yanga mara baada ya hivi karibuni kutangaza kutoa ndege kwa Yanga watakapokuwa wanakwenda kucheza fainali nchini Algeria dhidi ya USM Alger pamoja na kuongeza fedha ya goli la Mama mpaka milioni 20.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *