Rais Samia ashuhudia Tanzania ikipata msaada wa kibajeti na kimaendeleo kutoka Umoja wa Ulaya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Julai 04, 2023 ameshuhudia Utiaji Saini wa Mikataba Mitatu ya msaada uliotolewa na Umoja wa Ulaya (EU) yenye thamani ya Euro Milioni 179.35 sawa na Shilingi Bilioni 455.09 za Kitanzania na kupewa Msaada wa Bajeti ya Serikali kiasi cha Euro Milioni 46.11 sawa na Shilingi Bilioni 117.036 za Kitanzania kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 kutoka Umoja wa Ulaya.

Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma na mikataba hiyo imetiwa Saini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Umoja wa Ulaya hapa Nchini Mhe. Manfredo Fantl.

Fedha hizo za msaada kutoka Umoja wa Ulaya ni kwa ajili ya utekelezaji wa programu 3 za maendeleo na programu hizo 3 zitakazotekelezwa ni Uchumi wa Buluu, Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na uboreshaji wa mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa fedha za Serikali, pamoja kuwezesha sekta binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *