Rais Samia apokea andiko la Tanzania kuandaa AFCON 2027.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo Jumatano Mei 24, 2023 amepokea andiko la Ombi la Tanzania, Kenya na Uganda kuwa mwenyeji wa mashindano ya timu za Taifa za mpira (AFCON) mwaka 2027.

Andiko hilo amelipokea kutoka kwa Rais wa TFF Wallace Karia pamoja na Uongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Waziri wake Pindi Chana Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *