
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, jana Agosti 12, 2025, aliongoza viongozi, wanachama, wapenzi, wakereketwa wa CCM na Watanzania wapenda maendeleo katika harambee ya kuchangisha fedha, iliyolenga kukusanya kiasi cha Sh. bilioni 100 kwaajili ya kampeni za CCM za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambapo CCM ilikusanya Sh. bilioni 86.





