Rais Mwinyi kumwakilisha Rais Samia Jukwaa la Uchumi Qatar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar leo tarehe: 21 Mei 2023 kuelekea nchini Qatar kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi linalofanyika jijini Doha.

Jukwaa hilo linalodhaminiwa na Kampuni ya Kimataifa ya Bloomberg lenye kauli mbiu isemayo “ Simulizi za Ukuaji Kimataifa “ ambalo hufanyika nchini Qatar kila mwaka

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya washiriki ikiwa ni pamoja na viongozi wa kampuni kubwa duniani, viongozi wa juu wa Serikali, na pia mamlaka zinazohusika za Qatar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *