Rais Dkt. Samia aweka jiwe la msingi mradi wa Suluhu Sports Academy Kizimkazi

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Dkt, Samia Suluhu Hassan, leo ameweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa Suluhu Sports Academy mjini Kizimkazi, Zanzibar.

Mradi huo umejengwa na wadau wa Maendeleo wakiongozwa na CRDB Foundation ambapo ndani yake kutakuwa Viwanja vya Michezo mbalimbali ikiwemo Uwanja wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukuwa watazamaji 20,000.

Awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kukamilika Aprili, mwakani.

Uwekaji wa jiwe la msingi ni sehemu ya shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi 2024.

(Taarifa zaidi ya uzinduzi huo usikose kusoma Gazeti lako la Tanzania Leo ambalo lipo mtaani Jumatatu hadi Ijumaa)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *