Rais Dkt. Samia awasili Kenya kuhudhuria kampeni za Odinga kuwania Uenyekiti Kamisheni AU

Na Mwandishi Wetu, Nairobi

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 27, 2024 amewasili jijini Nairobi kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Raila Amolo Odinga ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya anayewania nafasi ya Mwenyekiti Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwa ni mualiko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo Dkt. William Samoei Ruto.

Hafla hiyo itafanyika katika Ikulu ya Nairobi na kuhudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali Agosti 27, 2024.

(Kwa taarifa zaidi usikose kusoma Gazeti lako la Tanzania Leo linalotoka kila Jumatatu hadi Ijumaa)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *