Na Mwandishi Wetu
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaongoza maelfu ya wananchi leo kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Dkt. Ndugulile alifariki dunia nchini India usiku wa kuamkia Novemba 27, mwaka huu alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kabla ya mwili kufika katika viwanja hivyo, leo asubuhi mwili huo ulipelekwa Kanisa la Mt. Immaculata-Upanga kwa ajili ya misa takatifu.
Zifutazo ni picha za matukio tofauti tofauti jinsi Rais Dkt. Samia alivyoshiriki;


