Rais Dkt. Samia afanya mazungumzo na Rais Xi Jinping wa China

Na Mwandishi Wetu, China

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mazungumzo na Rais wa China, Xi Jinping leo jijini Beijing baada ya kukutana na mwenyeji wake huyo katika Ukumbi wa The Great Hall of the People.

Mkutano huo pia ulimuhusisha Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema wakati wakishuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA katika ukumbi huo.

Katika mkutano huo, Rais Dkt. Samia alikuwa na ujumbe wake katika kikao hicho cha pamoja na Rais wa China, Xi Jinping ambaye pia alikuwa na ujumbe wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *