
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Rais wa Msumbiji Fransisco Chapo, yupo nchini kwa ziara ya siku tatu ambapo ametembelea Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kusifu jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo wenye viwango vya dunia.
Rais Chapo ameyasema wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua mradi huo ambapo alisafiri kutoka Shtesheninya Magufuli hadi Pugu ili kushuhudia viwango vya mradi huo aliouita wa kimataifa.

Naye Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amewasihi Watanzania kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuilinda na kuitunza miundombinu ya Reli ya Kisasa ya Umeme (SGR).
Prof. Mbarawa, ametoa wito huo katika stesheni ya Magufuli Dar es Salaaam, muda mchache baada ya kumsindikiza Rais Chapo, aliyesafiri kwa SGR kutoka Stesheni ya Magufuli kwenda stesheni ya Pugu na kisha kurejea stesheni ya Magufuli, kwa lengo kushuhudia mradi huo ambao ni wa kilelezo barani Afrika.

Prof. Mbarawa amesema Rais Chapo, aliyeko nchini kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu aliyoaianza Mei 07, 2028 ameeleza kufurahishwa na mradi huo aliosema ni wa kiwango cha dunia na kuwataka Watanzania, kuulinda kwa wivu.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Teli Tanzania (TRC) , Masanja Kadogosa, alisema kuwa ujio wa Rais Chapo ni ishara tosha ya kwamba Afrika inajua nini kinachoendelea Tanzania na pia kuzidi kudumisha mahusiano baina ya nchi za Afrika na kuimarisha katika ufanyaji biashara kwa ukaribu.

“Kikubwa zaidi katika nchi za Afrika ni kufanya biashara na wenzetu wa nchi nyingine wanatutazama tofauti na nchi ya Msumbiji tumekua tukishiriana katika Nyanja mbalimbali ikiwamo siasa, ulinzi na vilevile kijamii ukizungumza mmakonde wa Msumbiji na Tanzania hawana tofauti” amesema Kadogosa.





