NEC: Njooni mjiandikishe uboreshaji daftari la wapiga kura

Na Mwandishi Wetu, Tabora

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewaasa wakazi wa maeneo yaliyoteuliwa kwa majaribio ya uboreshaji wa katika zoezi hilo ambalo limelenga kupima utayari wa mifumo na vifaa vya uboreshaji wa daftari.

Mjumbe wa NEC, Balozi Omar Ramadhan Mapuri, aliyasema hayo wakati wa ufunguzi mkutano wa Tume na wadau wa uchaguzi uliofanyika mkoani Tabora jana.

Aliwapongeza wakazi wa Mkoa huo kuwa miongoni mwa mikoa miwili ambayo kata zake zimeteuliwa kufanya majaribio hayo kuanzia Novemba 24-30, 2023.

Alizitaja kata hizo ni Ng’ambo iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Kata ya Ikoma iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, mkoani Mara.

“Tume inawapongeza wakazi wa Tabora kwa Mkoa wenu kuteuliwa kuwa mwenyeji wa uboreshaji wa majaribio ya Daftari la Kudumu la Wapigakura,” alisema Mapuri.

Aliongeza kuwa, uboreshaji katika kata hizo utafanyika katika vituo 16 vya kuandikisha wapiga kura, vituo 10 Kata ya Ng’ambo, vituo sita Kata ya Ikoma.

Vituo vya uandikishaji vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *