Mwihambi : Bunge linamchango mkubwa Sekta ya Kilimo

Na Sarah Moses,Dodoma.

KATIBU wa Bunge Nenelwa Mwihambi amesema kuwa Bunge linamchango mkubwa katika sekta ya kilimo kwani kupitia Kamati za Bunge Wabunge wamekuwa wakitoa maoni na ushauri mbalimbali wa namna gani yakuboresha shughuli za kilimo  kwaajili ya manufaa ya nchi.

Hayo ameyasema leo Agosti 7,2024 Jijini Dodoma alipotembelea kwenye Maonesho ya Wakulima Nanenane ambapo amesema kuwa wao kama Bunge wamepata wageni wengi sana na hasa wanafunzi ambao wamekuja kujifunza shughuli mbalimbali ambazo zinahusiana na Bunge, nahivyo amewahamasisha wananchi wajitokeze kwani siku za maonesho bado zipo nyingi mpaka Agosti 10.

Amesema kuwa kama inavyofahamika Bunge kazi yake kuishauri serikali lakini na kuisimamia,bajeti inayofanyika kwenye shughuli hizi inatengwa na Bunge, lakini pia kupitia kwenye kamati za Bunge wabunge wamekuwa wakitoa maoni na ushauri mbalimbali wa namna gani ya kuboresha shughuli za kilimo kwaajili ya manufaa ya nchi yetu lakini na ajenda za nchi.

Lakini Pia kunamaswali ambayo yamekuwa yakiulizwa sana Bungeni na serikali inapata fursa ya kutoa maelezo mbalimbali na uhamasishaji umekuwa ukitolewa na wabunge ambao wanatoka kwenye maeneo ya kilimo.

“Maonyesho ya mwaka huu yamefana sana kwasababu muonekano wa huu uwanja wa Nanenane umebadilishwa kwa kiasi kikubwa kwani kwa ambao wanafahamu kulikuwa na vumbi,Barabara zilikuwa hazijakaa vizuri”amesema.

“Lakini mwaka huu Barabara zimejengwa vizuri,majengo yapo vizuri,kwahiyo kwaniaba ya  wafanyakazi wenzangu Ofisi ya Bunge tunawapongeza sana Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa uratibu mzuri ambao wamefanya”amesema Mwihambi.

mwisho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *