Mvua kubwa kunyesha siku 4 mfululizo

Na Salha Mohamed, Dar es Salaam

MVUA kubwa zinatarajiwa kunyesha kwa siku nne mfululizo kuanzia jana hadi Novemba 25,2023.

Mvua hizo huenda zinaleta madhara hata kusababisha vifo kama tahadhari hazitachukuliwa.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga, Unguja, Pemba, Mafia.

Athari zinazoweza kutokea ni pamoja na baadhi ya barabara kutopitika kutokana na mafuriko na vifo hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari.

TMA imetoa angalizo la mvua hizo kuendelea hadi Ijumaa na Jumamosi katika maeneo machache ya mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mafia, Unguja, Pemba.

Kwa mujibu wa TMA, Baadhi ya makazi yanaweza kujaa maji na kuathiri shughuli za kiuchumi,.

Agosti 26, 2023, TMA ilitoa taarifa ya uwezekano wa kuwepo mvua kubwa za El-Nino ambazo zinaweza kusababisha vif, magonjwa ya mlipuko, uharibifu wa miundombinu kuanzia Oktoba-Desemba, 2023.

TMA ilisema mvua hizo zitasababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi, upotevu wa mali, madhara ya kibinadamu pamoja na mazingira.

Kutokana na hali hiyo, TMA ilisishauri sekta na taasisi mbalimbali kuchukua hatua mapema kabla ya kuanza mvua hizo.

Sekta hizo ni kilimo, mifugo, uvuvi, utalii, uchukuzi, wanyamapori, mamlaka za miji, nishari, maji, madini, sekta binafsi, Wizara ya Afya, Menejimenti za maafa.

Awali kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Ladislaus Chang’a, alisema utabiri unaonyesha mvua hizo zitakuwa juu ya wastani na kushauri sekta mbalimbali nchini zijiandae kukabiliana na majanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *