MSD yawezeshwa na serikali kusambaza dawa, vifaa tiba Itilima – Simiyu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

SERIKALI kupitia Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Mwanza imeendelea kusambaza bidhaa za afya katika Mkoa wa Simiyu Wilaya ya Itilima.

Usambazaji huo unafanyika licha ya changamoto zinazosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo na nchini kwa ujumla.

Hatua hiyo ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suhulu Hasssan, kuhakikisha wananchi wanapata dawa na vifaa tiba kwa wakati bila kujali eneo wanaloishi lina vikwazo vya aina gani vya kimiundombinu.

Magari yenye vifaa tiba na dawa ya MSD yameendelea kutekeleza jukumu la kusamaza dawa katika barabara mbovu na mengine yakikwama, juduzi za kuwanasua zinaendelea ili yaweze kuendelea na safai.

Changamoto za aina hiyo na zaidi ya hizo zinazohatarisha maisha ya wafanyakazi wa MSD, imekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida kwa wafanyakazi wa bohari hiyo.

Lengo ni kuhakikisha Watanzania wanapata vifaa tiba na dawa kwa wakati ili kunusuru afya zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *