Mradi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere wafikia asilimia 87

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema mradi mkubwa na wa kimkakati wa kufua umeme kwa kutumia maji wa Bwawa la Mwalimu kwasasa umefikia asilimia 87, ukiwa kwenye hatua za mwisho mwisho kuelekea kukamilika kwake ifikapo Juni, 2024.

Mradi huo utazalisha takribani Megawatts 2,115 za umeme wa maji ambao ndiyo nafuu zaidi duniani miongoni mwa umeme na kulifanya Taifa kuwa na utoshelevu wa umeme na nafuu sana.

“Miradi mikubwa kama Mradi wetu wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, usipoenda kwenye misingi ya usimamizi na uendeshaji wa miradi, misingi ya ufundi na uhandisi pamoja na kusimamia uwajibikaji, lazima utakwama, sisi tuliamua kuyawekea mkazo hayo, na Kuhusu ratiba tulibadilisha mradi huu unafanyika usiku na mchana, weekend na sikukuu, tofauti na huko nyuma ambako Watu walifanya kazi kwa masaa 12 pekee pamoja na usimamizi mzuri wa Mkandarasi.

“Haya ni miongoni mwa mambo yaliyofanya mradi huu hadi sasa uko asilimia 87.” Alisema Waziri Makamba akizungumza na waandishi wa habari leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *