Mradi wa BRT kupitia PPP kubadili jiji la Dar

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Serikali imesaini mikataba na watoa huduma watatu kwaajili ya uendeshaji wa Awamu ya Pili ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) jijini Dar es Salaam, kupitia ubia na sekta binafsi (PPP) hatua inayolenga kuboresha usafiri wa umma.

Akitoa hotuba bungeni mjini Dodoma wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2025/26 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa, amesema hatua hiyo ni mwanzo wa zama mpya katika usafiri wa jiji.

“Kwa mara ya kwanza, tunasema: subira ya wananchi haikuwa ya bure. Tumefanikisha hatua ya kihistoria,” alisema Mchengerwa mbele ya wabunge.

Mchengerwa hakuweka wazi kampuni, gharama wala muda wa utekelezaji wa mikataba hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *