Michezo ya Spinners ‘Dubwi’ sasa kuchezwa mtandaoni kupitia betPawa

Na Mwandishi Wetu

KWA miaka mingi, ile ladha ya Spinners imekuwa ikiwavuta watu kwenye kasino za mtaani.

Yale makelele ya furaha, ule msisimko wa gurudumu likizunguka, na ule mchecheto wa kusubiri kuona kama ishara yako itatua mahali sahihi, hayo ndiyo maisha halisi ya kasino.

Hata hivyo, foleni, safari, na kusubiri kiti kunaweza kukatisha raha.

Kutokana na hali hiyo, chapa ya betPawa, kwa kushirikiana na Black Lagoon Games, wameleta michezo hiyo maarufu kwa jina la Dubwi moja kwa moja mtandaoni. Maboresho hayo ni mapinduzi mapya kabisa ya burudani, kwani sasa kasino yenyewe ipo kiganjani mwako.

Kwa sasa, mchezaji haitajiki tena kwenda kwenye kasino kucheza Spinner zake pendwa, kwani anaweza kucheza muda wowote na mahali popote kupitia simu ya mkononi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na betPawa na Black Lagoon Games, mapinduzi hayo yameletwa kwa lengo la kumrahisishia mchezaji kupata burudani akiwa sehemu yoyote hata akiwa safarini.

“Hakuna tena kusafiri au kugombania nafasi kwenye vyombo vya usafiri na kuingia gharama. Sasa unaweza kuingia mzigoni papo hapo na michezo kama Super Cup Spinner, Palm Beach Spinner, Car Show Spinner, Royal Tiger Spinner na Master League Spinner kiganjani,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefafanua zaidi kwamba, “Michezo hii yote iko mtandaoni, na unachotakiwa kufanya ni kubonyeza tu, kucheza na kuona matokeo papo hapo. Raha ya Dubwi bila kero.”
Cheza Rahisi, Lipwa Haraka!

Taarifa hiyo imesema kucheza Spinner mtandaoni kupitia betPawa ni rahisi kuliko unavyofikiria, kwani unaweza kucheza kwa pesa kidogo na malipo ni ya papo hapo.

Taarifa hiyo imewataka wachezaji wasiachwe nyuma kwenye mapinduzi haya ya michezo ya Spinner, huku ikiwataka kutembelea tovuti ya betPawa kupitia www.betpawa.co.tz/casino

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *