Na Suzanne Bearne
JENGO la lililoundwa kwa msururu wa safu za mianzi lenye urefu wa mita 19, katika shule ya Green School katika mji wa Bali linatajwa kama mojawapo ya majengo muhimu zaidi kuwahi kutengenezwa kutokana na mianzi.
Jengo hili lililoundwa na wasanifu majengo katika taasisi ya Ibuku na kutumia takriban tani 12.4 za miazi ya aina ya Dendrocalamus Asper, ambayo inajulikana pia kama Mwanzi Mbaya au Mwanzi Mkubwa, na muundo wake ulikamilishwa mnamo Aprili 2021.
Jengo kama hilo la kuvutia macho linaonyesha nguvu na ustadi wa mianzi. Ongezea kwenye kitambulisho cha kijani cha mianzi hiyo na itaonekana kama nyenzo bora kusaidia tasnia ya ujenzi kupunguza kiwango chake cha kaboni.
Ikiwa ni miti kama miti mingine, mimea ya mianzi hutenga kaboni inapokua na inaweza kufanya kazi kama mifereji ya kaboni, ikihifadhi kaboni zaidi kuliko spishi nyingi za miti.
Shamba la mianzi linaweza kuhifadhi tani 401 za kaboni kwa hekta (kwa ekari 2.5). Kinyume chake, shamba la miti ya misonobari ya Kichina linaweza kuhifadhi tani 237 za kaboni kwa hekta, kulingana na ripoti ya Shirika la Kimataifa la Mianzi na Rattan (INBAR) na Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Delft, nchini Uholanzi.
Ni moja ya mimea inayokua kwa kasi zaidi kwenye sayari – aina fulani hukua haraka kama mita moja kwa siku.
Zaidi ya hayo, mianzi ni nyasi, hivyo wakati shina linapovunwa huota tena, tofauti na miti mingi.
Ina historia ndefu ya kutumiwa shughuli za ujenzi barani Asia, lakini Ulaya na Marekani inabaki kuwa nyenzo za ujenzi.
Katika masoko hayo, mianzi iliyokaushwa kwa joto na kutiwa kemikali imekuwa ikitumika katika utengenezaji wa sakafu, meza za jikoni na mbao za kukatia, lakini haitumiki sana kama nyenzo za ujenzo
Kulingana na Christopher Matthews, kutoka kwa taasisi ya wahandisi wa miundo ya majengo yenye yake London – Atelier One, sehemu ya tatizo ni ukosefu wa ujuzi.
“Mojawapo ya changamoto kubwa ilikuwa hakuna mtu anayejua jinsi ya kujenga kwa mianzi,” anasema Bw Matthews, ambaye alifanya kazi katika mradi wa Shule ya Bali.
“Kwa hivyo tulilazimika kuipima. Tulikuwa pale, tukiipakia na mifuko ya mchanga ili kuthibitisha ina nguvu kiasi gani .”
Matthews anasema mahitaji ya mianzi yanaongezeka, huku 30% ya wateja wa kampuni yake sasa wakiitumia. “Tumeanza kutengeneza majengo ya mianzi zaidi na zaidi.”
Anaonyesha majengo yote ya shule huko New Mexico, na miundo kama vile studio ya yoga huko Costa Rica, na daraja na banda vilivyotengenezwa kwa mianzi nchini Ufilipino.
“Katika nchi zinazoitumia, mianzi ni nafuu sana na ni mingi mno, na wafanyakazi wana ujuzi katika kuitumia. Kama tungeanza kuitumia Ulaya, ingekuwa ghali zaidi. Lakini ikadri inavyoendelea kutumika zaidi na zaidi,” alisema, “basi hakuna sababu ya kutoshuka kwa gharama yake.”
Anasema kampuni iko katika mazungumzo ya hatua ya awali yatakayosaidia matumizi ya mianzi katika ujenzi nchini Uingereza hivi karibuni.
Ingesaidia kama mianzi ingekuzwa Ulaya, lakini spishi kubwa zaidi hazikui vizuri katika hali ya hewa baridi ya kaskazini.
Kampuni ya BambooLogic ambayo ni mkulima wa kwanza wa mianzi kwa kiwango kikubwa barani Ulaya inatarajia kubadilisha hilo.
“Kwa hakika, inahitaji jua zaidi, maji pia,” anasema Jan Detavernier, mshauri katika BambooLogic, ambayo ina mashamba ya mianzi nchini Ureno.
“Kusini, tuna jua jingi.” Anasema ina uwezo wa kurejesha rutuba katika udongo ulioharibika. “Tunapokua kusini mwa Ureno, udongo ni duni sana.
Kwa kuwa mianzi hufyonza hewa ya Kaboni diokside (CO2) na kuiweka ardhini, hufanya dunia kuwa bora zaidi.”
Detavernier anasema kampuni yake inafanya kazi na washirika ambao wanatengeneza bidhaa mpya kwa ajili ya soko la Ulaya.
Changamoto, anasema, ni ukosefu wa viwango. “Nchini Ulaya hatujazoea kufanya kuitumia mianzi kama nyenzo ya ujenzi. Kuna data nyingi barani Asia, lakini kuna data ndogo kuhusu matumizi yake katika ujenzi.”
Profesa msaidizi wa usanifu katika Shule ya Usanifu ya Chuo Kikuu cha Southern California, na pia mjumbe wa jopokazi linalounda viwango vya kimataifa vya vifaa vya ujenzi wa mianzi Dk Bhavna Sharma, anaunga mkono hili.
“Ni changamoto bado kutumia mianzi katika ujenzi kwasababu bado ni nyenzo isiyo ya kawaida,” anasema.
“Ni [kuhusu] tu kuongeza ujuzi wetu, kuelewa jinsi mianzi inavyoweza kufanya kazi katika mazingira tofauti ya huduma, ambayo inamaanisha ikiwa ninajenga Amsterdam, jengo linawezaje kuwa imara katika aina hiyo ya hali ya hewa na hali ya hewa ukilinganisha na jengo kama hilo iwapo litajengwa nchini Indonesia? Kwa njia hiyo tunaweza kusonga mbele zaidi kulingana na aina ya majengo ambayo tunaweza kuyajenga.”
Sharma anasema kwamba viwango vya kwanza vya kupima mianzi vilivyobuniwa kutoka Shirika la Viwango vya Kimataifa vilichapishwa msimu wa joto uliopita. “Hili litasaidia watendaji, wabunifu na wahandisi katika kuidhinisha mianzi katika miradi ya ujenzi.
Katika jimbo la California nchini Marekani, kampuni ya vifaa vya ujenzi endelevu ya BamCore, iliyoanzishwa mwaka wa 2019, inatoa mfumo wa uundaji wa vipande vya mianzi uliyobuniwa na mbao za mikaratusi. Vipande hivyo hutumika kujenga majengo yenye urefu wa hadi ghorofa tano za majengo ya biashara na makazi.
“Wateja wetu awali walianza kama wanunuzi wa nyumba moja au wasanifu,” anasema Kate Chilton, afisa mkuu wa uendelevu katika BamCore.
Kuna zaidi ya spishi 1,600 za mianzi, na inayopendekezwa na BamCore ni mianzi ya Dendrocalamus asper, ambayo huagizwa kutoka Amerika Kusini na Asia.
Hata hivyo, Bi Chilton anasema wako kwenye mazungumzo na mmiliki wa shamba la mianzi la Florida ambaye amekuwa akifanya majaribio endelevu ya ujenzi wa kutumia mianzi.
Baadhi ya watu wameanza kuukubali ubunifu wa mianzi. Kampuni ya mawakala wa huduma ya maandalizi ya matamasha, Natchlab, wamejenga jengo la mianzi lenye ukubwa wa mita 650-za duara kwa ajili ya Tamasha la Boom la sanaa na muziki nchini Ureno mwaka ujao.
“Mpango wa wazi, wenye uingizaji hewa wa kutosha, miundo ya juu ndiyo hasa unayohitaji katika tamasha,” Sibthorpe, mkurugenzi wa ubunifu wa Nachtlab, alisema katika mkutano wa Green – sehemu ya Tukio la Ngoma la Amsterdam.
“Muanzi unaweza kujipinda na kukatwa kidogo. Ni nyenzo inayoweza kutengenezwa.”
BBC