Mgeni asifu juhudi za wanawake kuinuana

NAIBU Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma, amesema ipo nguvu ya ziada iliyotumika kuhakikisha wanawake wanasoma masomo ya sayansi, kuongoza kampuni, taasisi na kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye siasa.

Ameyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye Jukwaa la Viongozi Wanawake, lililofanyika katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayofikia tamati leo Julai 13, 2024.

Amesema kuna dhana iliyokuwa imejengeka kuanzia ngazi ya familia kuwa, mwanamke hawezi kufanya kazi nyingine zaidi ya zile za nyumbani na kuolewa.

“Lakini wapo wanawake waliofanya kazi ya ziada kuhakikisha minyororo hiyo inakatika na wanawake wanaweza kufanya shughuli zilizokuwa zinaonekana ni za wanaume,” amesema Mgeni.

Amewataka wanawake viongozi hada vijana kutokatishwa tamaa na changamoto wanazokutana nazo hasa kwa kuzingatia wao walikutana na kubwa zaidi lakini hawakukata tamaa na kuendelea kusonga mbele.

Kadhalika amewataka wanawake kuzingatia kujiendeleza kielimu ili kuendelea kushika nafasi za juu za uongozi.
Mgeni pia alihimiza kuendelea kwa majukwaa hayo ambayo yanawatia moyo wanawake wengine kufikia malengo hayo.
Jukwaa hilo limeandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) na shirikisha wanawake viongozi kutoka taasisi binafsi na za umma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *