Messi aipeleka Inter Miami robo fainali

TEXAS, Marekani

BAO lililofungwa na nyota, Lionel Messi, limeisaidia timu yake ya Inter Miami kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Ligi kwa kuitandika FC Dallas jana asubuhi.

FC Dallas ilikuwa ikiongoza kwa mabao 4-2 hadi dakika 10 za mwisho lakini mabao mawili yaliyofungwa yalisababisha mchezo kwenda katika upigaji wa mikwaju ya penalti.

Miami ilishindwa kwa mikwaju 5-3 uwanjani Toyota mjini Frisco, Texas.

“Kuwa nyumba kwa mabao 4-2 katika dakika ya 80 na kisha kurudi mchezoni, tuna furaha sana na matokeo,” amesema Kocha wa Miami, Gerardo Martino.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *