Na Asha Kigundula
STRAIKA wa timu ya Azam FC, Mkongo Idris Mbombo, amesema watalipa kisasi katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Bahir Dar Kenema ya Ethiopia utakaopigwa Ijumaa kuanzia saa 1 usiku Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa kwanza, Azam ililambwa mabao 2-1 ugenini huku Mbombo akifunga bao pekee akitokea benchi.
Akizungumza Dar es Salaam jana kuelekea mchezo huo, Mbombo amesema kwa ufupi:” Tutawapiga mabao, karibuni kwa wingi Chamazi.
Azam ili kusonga mbele hatua inayofuata ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inatakiwa kushinda bao 1-0.
Timu hiyo pia kuelekea mchezo huo, imekuja na kauli mbiu ya ‘La Revancha!, ikimaanisha Kisasi.