MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Latifa Khamis amesema Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yamefanikiwa kwa asilimia 99.
Amesema washiriki kutoka mataifa mbalimbali wamekuja na kutamgaza fursa za uwekezaji ambao utasaidia kukuza sekta ya biashara nchini.
Latifa ameyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye Jukwaa la Viongozi Wanawake, lililofanyika katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayofikia tamati leo Julai 13, 2024
Amesema wanachi wengi wamejitokeza kutembelea maonesho hayo na hivyo kufanya kuwa na mvuto mkubwa.
“Wananchi waliojitokeza kutembelea mabanda mbalimbali ni wengi hususani siku ya Julai 7, yenyewe watu 50,000 walishiriki, haya ni mafanikio makubwa saha,” amesema Latifa.
Ameahidi kuwa wataendelea kuboresha maonesho hayo yaendelee kuwa yenye tija zaidi hasa kuwa lango la kufungua fursa za uchumi.