Wafanyabiashara wa Kariakoo kuanzia leo asubuhi wamekuwa kwenye mgomo kwa kufunga maduka wakiiomba Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuondoa utitiri wa kodi kwenye hilo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jioni hii amefika soko la Kariakoo kuzungumza na Wafanyabiashara kusikiliza kero zao baada ya mgomo mkubwa wa kufunga maduka ulioleta kero na kadhia kubwa kwa wanunuzi.
Waziri Mkuu amesimama Kariakoo kuzungumza na Wafanyabiashara ambapo moja ya kero zao kubwa ikiwemo kuwepo kwa vikosi kazi (task force) kutoka TRA vya kusumbua Wafanyabiashara na kuwakamata ameamuru kikosi hicho kusimama mara moja.
Majaliwa amesikiliza kero zao ambapo baada ya kupata kusikiliza Wafanyabiashara kupitia kwa Viongozi wao amesema watakutana na Wawakilishi wote wa Wafanyabiashara kwenye Ukumbi wa Anatoglo uliopo Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam ili kumaliza kero zote zinazowasumbua Wafanyabiashara ili soko la Kariakoo liendelee kuwa imara na la kimataifa.