Meneja wa Bandari Mkoa wa Tanga Masoud Mrisha amefafanua kuhusu faida za kukamilika kwa maboresho ya bandari hiyo leo kwa Wanahabari waliofika bandarini hapo na kujionea mabadiliko makubwa.
“Uwezo wa bandari kuhudumia meli kubwa mpaka hapa tunapozungumza baada ya huu mradi kukamilika tumeshaingiza meli sita zenye urefu wa mita 150 mpaka 200 kwa kipindi hiki cha miezi mitatu , shehena itaongezeka kutokana na kuhudumia meli kubwa.
“Kabla ya mradi tulikuwa na uwezo wa kuhudumia tani 750,000 lakini baada ya maboresho haya sasa tutakwenda mpaka tani milioni tatu kwa mwaka.
Kama nilivyoeleza kabla ya maboresho tulikuwa na gharama kubwa za uendeshaji kutokana na kufanya kazi mara mbili ya kupakua na kupakia, gharama za mafuta zimepungua.
“Hivyo gharama za uendeshaji zimepungua na faida ya tatu meli ambayo ilikuwa inahudumiwa kwa siku nane sasa inaweza kuhudumiwa kwa siku nne,” Alisema