Na Mwandishi Wetu
MASHABIKI wa soka wa Tanzania, sasa wanaweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwa pamoja na fedha kupitia Kampeni ya ‘Amsha Amsha’ iliyozinduliwa na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya M-Bet Tanzania na Halotel.
Kwa mujibu wa Meneja Masoko wa M-Bet, Levis Paul, amesema mbali ya zawadi ya fedha ya sh. 50,000 kwa washindi wawili kwa siku, pia mashabiki wa soka wanaweza kujishindia fedha taslimu, simu janja, na televisheni za kisasa.
Paul amesema kampeni hiyo imelenga kuwazawadia wateja wao ambapo pia wanaweza kushinda fedha kwa kubashiri matokeo ya mechi katika ligi mbalimbali duniani.
“Washindi wawili wa kila siku watajishindia sh. 50,000, ambapo jumla ya sh. 6,000,000 zimetengwa kwa kipindi hiki cha sikukuu,” amesema Paul.
Ameongeza kila mwisho wa wiki kutakuwa na droo maalum ambapo washindi wawili watajishindia simu janja ya Samsung A-Series yenye thamani ya sh. 500,000.
Zaidi ya hayo, wateja pia watapata nafasi ya kujishindia televisheni za kisasa aina ya Hisense zenye thamani ya sh. milioni 1.2 kila moja, ambapo jumla ya televisheni nane zitatolewa katika kipindi cha miezi mitatu ya promosheni.
Amesema shabiki wa soka anaweza kuingia kwenye droo kwa kujisajili kupitia tovuti yao, www.m-bet.co.tz, kuweka fedha kupitia HaloPesa na kubeti kwa dau la kuanzia sh. 2,000 ili kuingia kwenye droo.
Kwa upande wake, Ofisa Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza, amesema:“Tunafurahi kushirikiana na M-Bet kwenye promosheni hii. Lengo letu ni kutoa fursa kwa wateja kufurahia michezo ya kubashiri kupitia HaloPesa, ambayo ni njia rahisi na salama ya kufanya malipo. Promosheni hii itaunganisha burudani ya kubashiri na urahisi wa huduma za malipo ya simu.”
Lwiza ameongeza promosheni hiyo itawawezesha wateja wa HaloPesa kufurahia huduma za M-Bet na kuingia kwenye droo za zawadi za kila siku, wiki na mwezi.