M-Bet, HaloPesa wamwaga zawadi za washindi Kampeni ya ‘Amsha Amsha’

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya M-Bet kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Halotel kupitia HaloPesa, zimewazawadia washindi wa kwanza wa Kampeni ya ‘Amsha Amsha’ zawadi mbalimbali.

Meneja Masoko wa M-Bet, Levis Paul, amewataja washindi hao ni Ramadhan Mussa wa Dodoma na Greta Godfrey wa Dar es Salaam ambao wameshinda simu janja za mkononi aina ya Samsung A-series zenye thamani ya sh. 500,000  kila mmoja.

Mbali ya zawadi za simu za mkononi, pia Mkazi wa Songea, Vedasto Augustino, ameshinda televisheni aina ya Hisense yenye thamani ya sh. milioni 1.2.

Washindi wote wamekwisha patiwa zawadi zao ambapo, wakazi wa Dodoma na Songea wametumiwa kupitia utaratibu waliouweka.

Pia, Daniel Dende, Njelekela Vitass, Petro Edward, Manase Ernest, Paschaali Paulo, Joseph Kishala, January John, Yolanda George, Amani Yohana, Patrick Oswaldi, Esha Ally na Paul Lamson, wameshinda fedha taslimu sh. 50,000 kila mmoja.

Wengine walioshinda sh. 50,000 ni Alhaji Jabir, Frank Aidan, Amuri Hamisi, Yahaya Hamad, Siado Emmanuel, Rajab Chande, Kanisus Patrick, Mwasi Mwandito, Mashaka Kombo, Andrew Yohana na Saidi Mohamedi.

Mwakilishi wa Kampuni ya simu ya Halotel mkoani Dodoma, Jovita Minga (kushoto), akimkabidhi Ramadhan Mussa zawadi ya simu janja ya mkononi (smartphone) aina ya Samsung aliyoshinda kupitia Kampeni ya Amsha Amsha.

Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Levis Paul, amesema wanajisikia fahari kuwazawadia washindi hao zawadi hizo na kuwaomba kuendelea kushiriki kampeni hiyo ili kuendelea kushinda zawadi mbalimbali.

“Natoa wito kwa mashabiki wa soka na HaloPesa, kubashiri kuanzia dau la sh. 2,000 ili kuweza kushinda zawadi mbalimbali ikiwa pamoja zawadi ya fedha taslimu kwa washindi wawili kwa siku,” amesema Paul.

Paul amesema kampeni hiyo imelenga kuwazawadia wateja wao ambapo pia wanaweza kujishindia fedha kwa kubashiri matokeo ya mechi katika ligi mbalimbali duniani.

“Washindi wawili wa kila siku watajishindia sh. 50,000, ambapo jumla ya sh. 6,000,000 zimetengwa kwa kipindi hiki cha sikukuu, droo itafanyika kila mwisho wa wiki,” amesema Paul. 

Amesema hadi sasa sasa kuna televisheni saba ambazo zinasubiri washindi na kuwaomba mashabiki wa soka kuendelea kubashiri ili kushinda televisheni hizo na pia simu za kisasa za smartphone. 

Kampeni hiyo itadumu kwa muda wa  miezi mitatu.

Amefafanua shabiki wa soka au mteja wao anaweza kuingia kwenye droo kwa kujisajili kupitia tovuti, www.m-bet.co.tz, kuweka fedha kupitia HaloPesa na kubeti kwa dau la kuanzia sh. 2, 000 ili kuingia kwenye droo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *