Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI mpya ya kimataifa ya michezo ya kubashiri ya mitandaoni na kwenye Kasino ya LEONBET imeingia rasmi katika soko la Tanzania.
Kampuni hiyo ambayo inafanya shughuli zake katika nchi 19 duniani kote, tayari imepewa leseni ya kufanya shughuli zake nchini na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa LEONBET Tanzania, Tumaini Maligana, amethibitisha kupewa namba ya usajili SBI000000051 kwa ajili ya kuendesha michezo ya kubashiri ya mitandaoni na OCL00000027 kwa ajili ya kufanya shughuli za michezo ya Kasino.
Maligana amesema LEONBET inatoa huduma za kisasa zaidi na hiyo ndiyo sababu kubwa ya kupanua wigo na kuingia katika soko la Tanzania.
“LEONBET inalenga kuleta mapinduzi katika tasnia ya michezo ya kubashiri mtandaoni na kwenye kasino. Imejidhatiti kutoa huduma bora zaidi, uwepo wa kipekee mtandaoni na bonasi zinazovutia ili kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata thamani halisi ya fedha zao”.
“Kampuni hii ni ya kisasa zaidi na imejipanga kwa kukabiliana na ushindani wa michezo ya kubashiri ya mitandaoni na kwenye kasino kama tulivyofanya katika nchi nyingine 19 duniani,” amesema Maligana.
Amesema kwa zaidi ya miaka 15, LEONBET imekuwa ikitoa huduma bora za kubashiri michezo ya mitandaoni na ya Kasino kwa wateja wake na kuwavutia wengi.
Amefafanua LEONBET imeleta huduma rahisi na bora kwa wateja wa Tanzania na usajili wake ni rahisi sana.
“Ili kujisajili, unatakiwa kuwa na namba ya simu na neno la siri lako tu. Pia tunatoa njia rahisi za kuweka fedha na malipo ya haraka kupitia mitandao yote ya simu nchini. Huduma zetu kwa wateja zinapatikana kwa saa 24 kila siku na kukuwezesha kupata msaada wakati wowote unapohitaji,” amesema.
Kwa mujibu wa Malingana, mteja yeyote atakayejisajili na kuwa sehemu ya familia ya LEONBET, unapata sh. 2,000 bure kama ofa maalumu ya kujiunga, ambayo utaendelea kuipata kila unapoingia hadi mara nne kwa mwezi wa kwanza.